Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waefeso 5:3-4 - Compare All Versions

Waefeso 5:3-4 BHN (Biblia Habari Njema)

Kwa vile nyinyi ni watu wa Mungu, basi uasherati, uchafu wowote ule au choyo visitajwe kamwe miongoni mwenu. Tena maneno ya aibu, ya upuuzi au ubishi, yote hayo hayafai kwenu; maneno ya kumshukuru Mungu ndiyo yanayofaa.

Shirikisha
Waefeso 5 BHN

Waefeso 5:3-4 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru.

Shirikisha
Waefeso 5 SUV

Waefeso 5:3-4 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali kuwepo kushukuru.

Shirikisha
Waefeso 5 SRUV

Waefeso 5:3-4 NEN (Neno)

Lakini uasherati usitajwe miongoni mwenu kamwe, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu wa Mungu. Wala pasiwepo mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuzi au mzaha, ambayo hayafai, badala yake mshukuruni Mungu.

Shirikisha
Waefeso 5 NEN