Waefeso 5:21-24
Waefeso 5:21-24 Biblia Habari Njema (BHN)
Kila mmoja amstahi mwenzake kwa sababu ya heshima mliyo nayo kwa Kristo. Wake wawatii waume zao kama kumtii Bwana. Maana mume anayo mamlaka juu ya mkewe, kama vile Kristo alivyo na mamlaka juu ya kanisa; naye Kristo mwenyewe hulikomboa kanisa, mwili wake. Kama vile kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo, wake wawatii waume zao katika mambo yote.
Waefeso 5:21-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo. Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
Waefeso 5:21-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo. Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
Waefeso 5:21-24 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nyenyekeaneni ninyi kwa ninyi kwa heshima kwa ajili ya Kristo. Ninyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe kama vile Kristo alivyo kichwa cha Kanisa, ambalo ni mwili wake, naye Kristo ni Mwokozi wake. Basi, kama vile Kanisa linavyomtii Kristo, vivyo hivyo na wake nao imewapasa kuwatii waume zao kwa kila jambo.