Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waefeso 4:4-7 - Compare All Versions

Waefeso 4:4-7 BHN (Biblia Habari Njema)

Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile tumaini mliloitiwa na Mungu ni moja. Kuna Bwana mmoja, imani moja na ubatizo mmoja; kuna Mungu mmoja na Baba wa wote, ambaye yuko juu ya wote, afanya kazi katika yote na yuko katika yote. Kila mmoja wetu amepewa neema kadiri ya kipimo alichojaliwa na Kristo.

Shirikisha
Waefeso 4 BHN

Waefeso 4:4-7 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote. Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.

Shirikisha
Waefeso 4 SUV

Waefeso 4:4-7 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Kuna mwili mmoja, na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote. Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.

Shirikisha
Waefeso 4 SRUV

Waefeso 4:4-7 NEN (Neno)

Kuna mwili mmoja na Roho mmoja, kama vile mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Tena kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja, Mungu mmoja ambaye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote, katika yote na ndani ya yote. Lakini kila mmoja wetu amepewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa cha Kristo.

Shirikisha
Waefeso 4 NEN