Mhubiri 7:5-7
Mhubiri 7:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Afadhali kusikia maonyo ya wenye hekima kuliko kusikiliza nyimbo za wapumbavu. Maana, kicheko cha mpumbavu ni kama mlio wa miiba motoni. Hayo nayo ni bure kabisa. Mwenye hekima akimdhulumu mtu; hujifanya mwenyewe kuwa mpumbavu kupokea rushwa hupotosha akili.
Mhubiri 7:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Heri kusikia laumu ya wenye hekima, Kuliko mtu kusikia wimbo wa wapumbavu; Maana kama mlio wa miiba chini ya sufuria, Ndivyo kilivyo kicheko cha mpumbavu. Hayo nayo ni ubatili. Kweli jeuri humpumbaza mwenye hekima, Na rushwa huuharibu ufahamu.
Mhubiri 7:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Heri kusikia laumu ya wenye hekima, Kuliko mtu kusikia wimbo wa wapumbavu; Maana kama mlio wa miiba chini ya sufuria, Ndivyo kilivyo kicheko cha mpumbavu. Hayo nayo ni ubatili. Kweli jeuri humpumbaza mwenye hekima, Na rushwa huuharibu ufahamu.
Mhubiri 7:5-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Afadhali kusikia karipio la mtu mwenye hekima, kuliko kusikiliza wimbo wa wapumbavu. Kama ilivyo kuvunjika kwa miiba chini ya sufuria, ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu. Hili nalo pia ni ubatili. Dhuluma humfanya mtu mwenye hekima kuwa mpumbavu, nayo rushwa huuharibu moyo.