Mhubiri 7:1-6
Mhubiri 7:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Sifa njema ni bora kuliko marashi ya thamani. Siku ya kufa ni bora kuliko siku ya kuzaliwa. Afadhali kwenda kwenye matanga, kuliko kwenda kwenye karamu, kwa sababu walio hai yawapasa kukumbuka kwamba kifo chatungojea sisi sote. Huzuni ni afadhali kuliko kicheko maana, huzuni ya uso ni faida ya moyo. Moyo wa mwenye hekima huthamini matanga, lakini moyo wa mpumbavu hupenda raha. Afadhali kusikia maonyo ya wenye hekima kuliko kusikiliza nyimbo za wapumbavu. Maana, kicheko cha mpumbavu ni kama mlio wa miiba motoni. Hayo nayo ni bure kabisa.
Mhubiri 7:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Heri sifa njema kuliko manukato ya thamani; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa. Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake. Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo. Moyo wake mwenye hekima umo nyumbani mwa matanga, bali moyo wake mpumbavu umo nyumbani mwa furaha. Heri kusikia laumu ya wenye hekima, Kuliko mtu kusikia wimbo wa wapumbavu; Maana kama mlio wa miiba chini ya sufuria, Ndivyo kilivyo kicheko cha mpumbavu. Hayo nayo ni ubatili.
Mhubiri 7:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Heri sifa njema kuliko marhamu nzuri; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa. Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake. Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, Maana simanzi ya uso ni faida ya moyo. Moyo wake mwenye hekima umo nyumbani mwa matanga, bali moyo wake mpumbavu umo nyumbani mwa furaha. Heri kusikia laumu ya wenye hekima, Kuliko mtu kusikia wimbo wa wapumbavu; Maana kama mlio wa miiba chini ya sufuria, Ndivyo kilivyo kicheko cha mpumbavu. Hayo nayo ni ubatili.
Mhubiri 7:1-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Afadhali sifa nzuri kuliko manukato safi, nayo siku ya kufa kuliko ya kuzaliwa. Afadhali kwenda kwenye nyumba ya msiba kuliko kwenda kwenye nyumba ya karamu, kwa kuwa kifo ni hatima ya kila mwanadamu, imewapasa walio hai kuliweka hili mioyoni mwao. Huzuni ni afadhali kuliko kicheko, kwa sababu uso wenye huzuni wafaa kwa moyo. Moyo wa wenye hekima uko katika nyumba ya msiba, lakini moyo wa wapumbavu uko katika nyumba ya anasa. Afadhali kusikia karipio la mtu mwenye hekima, kuliko kusikiliza wimbo wa wapumbavu. Kama ilivyo kuvunjika kwa miiba chini ya sufuria, ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu. Hili nalo pia ni ubatili.