Mhubiri 7:1-2
Mhubiri 7:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Sifa njema ni bora kuliko marashi ya thamani. Siku ya kufa ni bora kuliko siku ya kuzaliwa. Afadhali kwenda kwenye matanga, kuliko kwenda kwenye karamu, kwa sababu walio hai yawapasa kukumbuka kwamba kifo chatungojea sisi sote.
Mhubiri 7:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Heri sifa njema kuliko manukato ya thamani; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa. Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake.
Mhubiri 7:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Heri sifa njema kuliko marhamu nzuri; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa. Heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni mwake.
Mhubiri 7:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Afadhali sifa nzuri kuliko manukato safi, nayo siku ya kufa kuliko ya kuzaliwa. Afadhali kwenda kwenye nyumba ya msiba kuliko kwenda kwenye nyumba ya karamu, kwa kuwa kifo ni hatima ya kila mwanadamu, imewapasa walio hai kuliweka hili mioyoni mwao.