Mhubiri 5:8-9
Mhubiri 5:8-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Usishangae ukiona katika nchi watu fukara wanakandamizwa, wananyimwa haki zao na maslahi yao. Kila mwenye cheo anayewadhulumu wanyonge yupo chini ya mkuu mwingine, na juu ya hao wote kuna wakuu zaidi. Hata hivyo, mfalme akijishughulisha na kilimo ni manufaa kwa wananchi wote.
Mhubiri 5:8-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, Aliye Juu kuliko walio juu huangalia; Tena wako walio juu kupita hao. Lakini, pamoja na hayo, manufaa ya nchi kwa kila njia ni mfalme anayejibidiisha kwa ajili ya shamba.
Mhubiri 5:8-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, Aliye juu kuliko walio juu huangalia; Tena wako walio juu kupita hao. Lakini, pamoja na hayo, manufaa ya nchi kwa kila njia ni mfalme anayejibidiisha kwa ajili ya shamba.
Mhubiri 5:8-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ukiona maskini wanaodhulumiwa katika nchi, na hukumu na haki vikipotoshwa, usishangazwe na mambo hayo; kwa maana afisa mmoja anaangaliwa na aliye juu yake, na juu ya hao wawili kuna wengine walio juu yao. Mafanikio ya nchi ni kwa ajili ya wote, hata mfalme mwenyewe hufaidi kutoka mashambani.