Mhubiri 4:4-6
Mhubiri 4:4-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Tena niligundua kwamba juhudi zote za mtu na ujuzi wake katika kazi vyatokana na kuoneana wivu. Hayo nayo ni bure kabisa; ni sawa na kufukuza upepo. Mpumbavu hafanyi kazi na mwisho hujiua kwa njaa. Ni afadhali kuwa na kidogo tu, pamoja na amani moyoni, kuliko kuwa na mengi, pamoja na taabu; sawa tu na kufukuza upepo.
Mhubiri 4:4-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena nikagundua kuwa juhudi zote, na ustadi wote katika kazi, hutokana na mtu kumwonea mwingine wivu. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo. Mpumbavu huikunja mikono yake, Naye hula chakula chake mwenyewe; Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kufukuza upepo.
Mhubiri 4:4-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena nikafikiri amali zote, na kila kazi ya ustadi, ya kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo. Mpumbavu huikunja mikono yake, Naye hula chakula chake mwenyewe; Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo.
Mhubiri 4:4-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Tena nikaona kuwa kazi zote na mafanikio yote huchipuka kutokana na wivu wa mtu kwa jirani yake. Hili nalo ni ubatili, ni kukimbiza upepo. Mpumbavu hukunja mikono yake na kujiangamiza mwenyewe. Afadhali konzi moja pamoja na utulivu kuliko konzi mbili pamoja na taabu na kukimbiza upepo.