Mhubiri 4:1-7
Mhubiri 4:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha nikaona udhalimu wote unaofanyika duniani. Watu wanaokandamizwa hulia machozi, lakini hakuna yeyote anayewafariji. Wakandamizaji wao wana nguvu, ndiyo sababu hakuna wa kuwafariji. Basi, nikafikiri moyoni kuwa wafu waliokwenda wasikorudi, wana nafuu zaidi kuliko watu walio hai. Lakini ana heri zaidi kuliko wafu na walio hai, yule ambaye bado hajazaliwa na kuona maovu yote yanayotendwa hapa duniani. Tena niligundua kwamba juhudi zote za mtu na ujuzi wake katika kazi vyatokana na kuoneana wivu. Hayo nayo ni bure kabisa; ni sawa na kufukuza upepo. Mpumbavu hafanyi kazi na mwisho hujiua kwa njaa. Ni afadhali kuwa na kidogo tu, pamoja na amani moyoni, kuliko kuwa na mengi, pamoja na taabu; sawa tu na kufukuza upepo. Tena, niliona jambo moja bure kabisa duniani.

Mhubiri 4:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha nikarudi na kuona udhalimu wote unaotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, lakini wale walikuwa hawana mfariji. Kwa hiyo nikawasifu wafu waliokwisha kufa kuliko wenye uhai walio hai bado; naam, zaidi ya hao wote nikamwita heri yeye asiyekuwako bado, ambaye hakuyaona mabaya yanayotendeka chini ya jua. Tena nikagundua kuwa juhudi zote, na ustadi wote katika kazi, hutokana na mtu kumwonea mwingine wivu. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo. Mpumbavu huikunja mikono yake, Naye hula chakula chake mwenyewe; Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kufukuza upepo. Kisha nikarudi tena, na kuona ubatili chini ya jua.
Mhubiri 4:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha nikarudi na kuona madhalimu yote yanayotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, walakini wale walikuwa hawana mfariji. Kwa hiyo nikawasifu wafu waliokwisha kufa kuliko wenye uhai walio hai bado; naam, zaidi ya hao wote nikamwita heri yeye asiyekuwako bado, ambaye hakuyaona mabaya yanayotendeka chini ya jua. Tena nikafikiri amali zote, na kila kazi ya ustadi, ya kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo. Mpumbavu huikunja mikono yake, Naye hula chakula chake mwenyewe; Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kujilisha upepo. Kisha nikarudi tena, na kuona ubatili chini ya jua.
Mhubiri 4:1-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nikatazama tena nikaona uonevu wote uliokuwa unafanyika chini ya jua: Nikaona machozi ya waliodhulumiwa, wala hawana mfariji; uwezo ulikuwa upande wa wale wanaowadhulumu, lakini hawakuwa na mfariji. Nami nikasema kwamba wafu, waliokwisha kufa, wana furaha kuliko watu walio hai, ambao bado wanaishi. Lakini aliye bora kuliko hao wawili ni yule ambaye hajazaliwa bado, ambaye hajaona ule uovu unaofanyika chini ya jua. Tena nikaona kuwa kazi zote na mafanikio yote huchipuka kutokana na wivu wa mtu kwa jirani yake. Hili nalo ni ubatili, ni kukimbiza upepo. Mpumbavu hukunja mikono yake na kujiangamiza mwenyewe. Afadhali konzi moja pamoja na utulivu kuliko konzi mbili pamoja na taabu na kukimbiza upepo. Tena nikaona kitu kingine kilicho ubatili chini ya jua