Mhubiri 4:1-3
Mhubiri 4:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha nikaona udhalimu wote unaofanyika duniani. Watu wanaokandamizwa hulia machozi, lakini hakuna yeyote anayewafariji. Wakandamizaji wao wana nguvu, ndiyo sababu hakuna wa kuwafariji. Basi, nikafikiri moyoni kuwa wafu waliokwenda wasikorudi, wana nafuu zaidi kuliko watu walio hai. Lakini ana heri zaidi kuliko wafu na walio hai, yule ambaye bado hajazaliwa na kuona maovu yote yanayotendwa hapa duniani.
Mhubiri 4:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha nikarudi na kuona udhalimu wote unaotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, lakini wale walikuwa hawana mfariji. Kwa hiyo nikawasifu wafu waliokwisha kufa kuliko wenye uhai walio hai bado; naam, zaidi ya hao wote nikamwita heri yeye asiyekuwako bado, ambaye hakuyaona mabaya yanayotendeka chini ya jua.
Mhubiri 4:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha nikarudi na kuona madhalimu yote yanayotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, walakini wale walikuwa hawana mfariji. Kwa hiyo nikawasifu wafu waliokwisha kufa kuliko wenye uhai walio hai bado; naam, zaidi ya hao wote nikamwita heri yeye asiyekuwako bado, ambaye hakuyaona mabaya yanayotendeka chini ya jua.
Mhubiri 4:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nikatazama tena nikaona uonevu wote uliokuwa unafanyika chini ya jua: Nikaona machozi ya waliodhulumiwa, wala hawana mfariji; uwezo ulikuwa upande wa wale wanaowadhulumu, lakini hawakuwa na mfariji. Nami nikasema kwamba wafu, waliokwisha kufa, wana furaha kuliko watu walio hai, ambao bado wanaishi. Lakini aliye bora kuliko hao wawili ni yule ambaye hajazaliwa bado, ambaye hajaona ule uovu unaofanyika chini ya jua.