Mhubiri 2:24-26
Mhubiri 2:24-26 Biblia Habari Njema (BHN)
Hakuna chema kimfaacho binadamu, isipokuwa kula na kunywa na kuifurahia kazi yake. Hili nalo nimeliona kuwa latoka kwa Mungu, maana usipojaliwa na Mungu, huwezi kupata chakula wala kujifurahisha. Mungu humjalia mtu apendezwaye naye hekima, akili na furaha; lakini humpa mwenye dhambi kazi ya kuvuna na kurundika, kisha akampa anayempendeza yeye Mungu. Yote hayo pia ni bure kabisa; ni sawa na kufukuza upepo.
Mhubiri 2:24-26 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwanadamu hapati jema kupita kula na kunywa, na kuiburudisha roho yake kwa mema katika kazi yake. Hayo nayo niliona ya kwamba hutoka mkononi mwa Mungu. Kwa maana ni nani awezaye kula au kujiburudisha kuliko mimi? Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.
Mhubiri 2:24-26 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwanadamu hapati jema kupita kula na kunywa, na kuiburudisha roho yake kwa mema katika kazi yake. Hayo nayo naliona ya kwamba hutoka mkononi mwa Mungu. Kwa maana ni nani awezaye kula au kujiburudisha kuliko mimi? Kwa sababu Mungu humpa yeye aliyemridhia hekima na maarifa na furaha; bali mkosaji humpa taabu, ili kukusanya na kututa, apate kumpa huyo ambaye Mungu amridhia. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo.
Mhubiri 2:24-26 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hakuna kitu bora anachoweza kufanya mtu zaidi ya kula na kunywa na kuridhika katika kazi yake. Hili nalo pia, ninaona, latokana na mkono wa Mungu, kwa sababu pasipo yeye, ni nani awezaye kula na kufurahi? Kwa yule mtu anayempendeza Mungu, Mungu humpa hekima, maarifa na furaha, bali kwa mwenye dhambi Mungu humpa kazi ya kukusanya na kuhifadhi utajiri ili Mungu ampe yule anayempenda. Hili nalo pia ni ubatili, ni kukimbiza upepo.