Mhubiri 12:5-7
Mhubiri 12:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Wakati huo utaogopa kupanda mahali pa juu na kutembea barabarani ni kitisho; wakati miti ya mlozi inachanua na panzi wanashiba, lakini wewe hutakuwa na hamu tena. Wakati huo binadamu anapaswa kwenda katika makao yake ya milele, nao waombolezaji watapitapita barabarani. Wakati huo uzi wa dhahabu utakatika, bakuli la dhahabu litapasuka, mtungi wa maji utavunjikia kisimani, kadhalika na gurudumu la kuvutia maji. Nawe vumbi utarudia udongoni ulimotolewa na roho yako itamrudia Mungu aliyeiumba.
Mhubiri 12:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naam, wataogopa kilichoinuka Na vitisho vitakuwapo njiani; Na mlozi utachanua maua; Na panzi atakuwa ni mzigo mzito; Na pilipili hoho itapasuka; Maana mtu aiendea nyumba yake ya milele, Nao waombolezao wazunguka njiani. Kabla haijakatika kamba ya fedha; Au kuvunjwa bakuli la dhahabu; Au mtungi kuvunjika kisimani; Au gurudumu kuvunjika birikani; Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
Mhubiri 12:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naam, wataogopa kilichoinuka Na vitisho vitakuwapo njiani; Na mlozi utachanua maua; Na panzi atakuwa ni mzigo mzito; Na pilipili hoho itapasuka; Maana mtu aiendea nyumba yake ya milele, Nao waombolezao wazunguka njiani. Kabla haijakatika kamba ya fedha; Au kuvunjwa bakuli la dhahabu; Au mtungi kuvunjika kisimani; Au gurudumu kuvunjika birikani; Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, Nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa.
Mhubiri 12:5-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
wakati watu watakapoogopa kilichoinuka juu na hatari zitakazokuwepo barabarani; wakati mlozi utakapochanua maua na panzi kujikokota nawe usiwe na shauku ya kitu chochote. Ndipo mwanadamu aiendea nyumba yake ya milele nao waombolezaji wakizunguka barabarani. Mkumbuke Muumba wako: kabla haijakatika kamba ya fedha, au bakuli la dhahabu halijavunjika; kabla mtungi kuvunjika kwenye chemchemi, au gurudumu kuvunjika kisimani, nayo mavumbi kurudi ardhini yalikotoka, na roho kurudi kwa Mungu aliyeitoa.