Mhubiri 11:7-10
Mhubiri 11:7-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwanga wafaa, na kuliona jua kwapendeza macho. Mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie miaka hiyo yote; lakini akumbuke kuwa siku za giza zitakuwa nyingi, na kwamba yote yatakayofuata ni bure. Ewe kijana, furahia ujana wako, moyo wako, uchangamke wakati ungali kijana. Fuata mapenzi ya moyo wako na upeo wa macho yako. Lakini kumbuka kwamba Mungu atakuhukumu kadiri ya hayo yote. Ondoa mahangaiko moyoni mwako, jikinge, usipate maumivu mwilini kwa sababu ujana na mwisho wa maisha ni bure kabisa.
Mhubiri 11:7-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kweli nuru ni tamu, tena ni jambo la kupendeza macho kutazama jua. Naam, mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote; lakini na azikumbuke siku zijazo za giza, kwa maana zitakuwa nyingi. Mambo yote yajayo ni ubatili. Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na kinachotamaniwa na macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni. Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini mwako; kwa maana ujana ni ubatili, na utu uzima pia.
Mhubiri 11:7-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kweli nuru ni tamu, tena ni jambo la kupendeza macho kutazama jua. Naam, mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote; lakini na azikumbuke siku zijazo za giza, kwa maana zitakuwa nyingi. Mambo yote yajayo ni ubatili. Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni. Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini mwako; kwa maana ujana ni ubatili, na utu uzima pia.
Mhubiri 11:7-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Nuru ni tamu, tena inafurahisha macho kuona jua. Mtu akiishi miaka mingi kiasi gani, na aifurahie yote. Lakini akumbuke siku za giza, kwa maana zitakuwa nyingi. Kila kitu kitakachokuja ni ubatili. Furahi ewe kijana, ukiwa bado kijana, moyo wako na ukupe furaha siku za ujana wako. Fuata njia za moyo wako na chochote macho yako yanaona, lakini ujue kwamba kwa ajili ya haya yote Mungu atakuleta hukumuni. Kwa hiyo, ondoa wasiwasi moyoni mwako na utupilie mbali masumbufu ya mwili wako, kwa kuwa ujana na nguvu ni ubatili.