Mhubiri 10:8-11
Mhubiri 10:8-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Mchimba shimo hutumbukia mwenyewe, abomoaye ukuta huumwa na nyoka. Mchonga mawe huumizwa nayo, mkata kuni hukabiliwa na hatari. Nguvu nyingi zaidi zahitajika kwa mtumiaji shoka butu lisilonolewa, lakini kutumia hekima humfanya mtu afanikiwe. Nyoka akiuma kabla hajachochewa, mchochezi hahitajiki tena.
Mhubiri 10:8-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma. Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo; Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo. Iwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi; Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi. Lakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa. Nyoka akiuma kabla hajachezeshwa, Basi hakuna faida ya mchezeshaji.
Mhubiri 10:8-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma. Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo; Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo. Iwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi; Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi. Walakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa. Nyoka akiuma asijatumbuizwa, Basi hakuna faida ya mtumbuizi.
Mhubiri 10:8-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Yeye achimbaye shimo aweza kutumbukia ndani yake, yeyote abomoaye ukuta anaweza kuumwa na nyoka. Yeyote apasuaye mawe inawezekana yakamuumiza, yeyote apasuaye magogo inawezekana yakamuumiza. Kama shoka ni butu na halikunolewa, nguvu nyingi zinahitajika, lakini ustadi utaleta mafanikio. Nyoka akiuma kabla ya kuchezeshwa, mchezeshaji hatahitajika tena.