Mhubiri 10:5-7
Mhubiri 10:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Kuna uovu niliogundua hapa duniani, uovu unaosababishwa na watawala: Kwamba wapumbavu wanapewa kazi za madaraka ya juu, na matajiri wanachukua nafasi za mwisho. Nimeona watumwa wanapanda farasi, na wakuu wanatembea kwa miguu kama watumwa.
Mhubiri 10:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye; ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini. Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.
Mhubiri 10:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye; ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini. Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.
Mhubiri 10:5-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kuna ubaya niliouona chini ya jua, aina ya kosa litokalo kwa mtawala: Wapumbavu kuwekwa kwenye nafasi nyingi za utawala, hali matajiri wanashika nafasi za chini. Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, wakati wakuu wakitembea kwa miguu kama watumwa.