Kumbukumbu la Sheria 5:9-10
Kumbukumbu la Sheria 5:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
“ ‘Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wale wanichukiao. Lakini nawafadhili maelfu ya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.
Kumbukumbu la Sheria 5:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
Kumbukumbu la Sheria 5:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
Kumbukumbu la Sheria 5:9-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, BWANA Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanaonichukia, lakini ninaonesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanaonipenda na kuzishika amri zangu.