Kumbukumbu la Sheria 4:7-8
Kumbukumbu la Sheria 4:7-8 Biblia Habari Njema (BHN)
“Hakuna taifa lolote hata liwe kuu namna gani, ambalo mungu wake yuko karibu nalo, kama alivyo karibu nasi Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, tunapomwomba msaada. Wala hakuna taifa lingine lolote hata liwe kuu namna gani, lenye masharti na maagizo ya haki, kama hayo ambayo nimewafundisha siku hii ya leo.
Kumbukumbu la Sheria 4:7-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama BWANA Mungu wetu alivyo kila tumwitapo? Tena liko taifa gani kubwa, lililo na amri na hukumu zenye haki kama torati hii yote, ninayoiweka mbele yenu leo?
Kumbukumbu la Sheria 4:7-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama BWANA, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo? Tena liko taifa gani kubwa, lililo na amri na hukumu zenye haki kama torati hii yote, ninayoiweka mbele yenu leo.
Kumbukumbu la Sheria 4:7-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ni taifa gani jingine lililo kubwa kiasi cha kuwa na miungu yao iliyo karibu nao kama BWANA Mungu wetu alivyo karibu nasi wakati wowote tunapomwomba? Nalo ni taifa gani jingine lililo kubwa hivi lenye kuwa na amri na sheria za haki kama hizi ninazoweka mbele yenu leo?