Kumbukumbu la Sheria 4:48-49
Kumbukumbu la Sheria 4:48-49 Biblia Habari Njema (BHN)
Nchi hiyo ilienea toka Aroeri ukingoni mwa mto Arnoni, hadi mlima Sirioni yaani Hermoni, pamoja na eneo lote mashariki ya mto Yordani mpaka bahari ya Araba, mwishoni mwa miteremko ya mlima Pisga.
Kumbukumbu la Sheria 4:48-49 Swahili Revised Union Version (SRUV)
toka Aroeri, iliyo juu ya ukingoni pa bonde la Arnoni, hadi mlima wa Sioni (nao ndio Hermoni), na Araba yote iliyo ng'ambo ya Yordani upande wa mashariki, hata mpaka bahari ya Araba, chini ya materemko ya Pisga.
Kumbukumbu la Sheria 4:48-49 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
toka Aroeri, iliyo juu ya ukingoni pa bonde la Arnoni, hata mpaka mlima wa Sioni (nao ndio Hermoni), na Araba yote iliyo ng’ambo ya Yordani upande wa mashariki, hata mpaka bahari ya Araba, chini ya matelemko ya Pisga.
Kumbukumbu la Sheria 4:48-49 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Nchi hii ilienea kutoka Aroeri ukingoni mwa Bonde la Arnoni hadi Mlima Sioni (yaani Hermoni), pamoja na eneo lote la Araba mashariki mwa Yordani, na kuenea hadi Bahari ya Araba kwenye miteremko ya Pisga.