Kumbukumbu la Sheria 4:35-36
Kumbukumbu la Sheria 4:35-36 Biblia Habari Njema (BHN)
Nyinyi mlijaliwa kuyaona mambo hayo, ili mpate kutambua kwamba Mwenyezi-Mungu, ndiye peke yake Mungu na wala hakuna mwingine. Aliwafanya muisikie sauti yake kutoka mbinguni ili aweze kuwafunza nidhamu; na hapa duniani akawafanya mwone moto wake mkubwa na kusikia maneno yake kutoka katikati ya moto huo.
Kumbukumbu la Sheria 4:35-36 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wewe umeoneshwa haya, ili upate kujua ya kuwa BWANA ndiye Mungu, hapana mwingine ila yeye. Kutoka mbinguni amekufanya usikie sauti yake, ili akufundishe; na juu ya nchi alikuonesha moto wake mkuu; ukasikia maneno yake kutoka katika moto.
Kumbukumbu la Sheria 4:35-36 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wewe umeonyeshwa haya, ili upate kujua ya kuwa BWANA ndiye Mungu, hapana mwingine ila yeye. Kutoka mbinguni amekusikizisha sauti yake, ili akufundishe; na juu ya nchi alikuonyesha moto wake mkuu; ukasikia maneno yake toka kati ya moto.
Kumbukumbu la Sheria 4:35-36 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Mlioneshwa mambo haya ili mpate kujua kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu; hakuna mwingine ila yeye. Kutoka mbinguni amewasikizisha sauti yake ili kuwaadilisha. Hapa duniani aliwaonesha moto wake mkubwa, nanyi mlisikia maneno yake kutoka kati ya ule moto.