Kumbukumbu la Sheria 33:2
Kumbukumbu la Sheria 33:2 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu alikuja kutoka mlima Sinai, alitutokea kutoka mlima Seiri; aliiangaza kutoka mlima Parani. Alitokea kati ya maelfu ya malaika, na moto uwakao katika mkono wake wa kulia.
Kumbukumbu la Sheria 33:2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawajia kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kulia Palikuwa na sheria ya motomoto kwao.
Kumbukumbu la Sheria 33:2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawaondokea kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kuume Palikuwa na sheria ya moto-moto kwao.
Kumbukumbu la Sheria 33:2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Alisema: “BWANA alikuja kutoka Mlima Sinai, akachomoza kama jua juu yao kutoka Mlima Seiri, akaangaza kutoka Mlima Parani. Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu kutoka kusini, kutoka materemko ya mlima wake.