Kumbukumbu la Sheria 15:10-11
Kumbukumbu la Sheria 15:10-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Mpeni ndugu maskini kwa ukarimu bila kunungunika; maana kwa ajili ya hayo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawabariki katika kazi zenu zote na katika kila mfanyalo. Maana maskini hawatakosekana nchini; hivyo nawaamuru, muwe wakarimu kwa ndugu zenu wahitaji na maskini nchini mwenu.
Kumbukumbu la Sheria 15:10-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mpe kwa kweli, wala moyo wako usisikitike utakapompa; kwa kuwa atakubarikia BWANA, Mungu wako, kwa neno hili katika kazi yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako. Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako.
Kumbukumbu la Sheria 15:10-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mpe kwa kweli, wala moyo wako usisikitike utakapompa; kwa kuwa atakubarikia BWANA, Mungu wako, kwa neno hili katika kazi yako yote, na katika kila utakalotia mkono wako. Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako.
Kumbukumbu la Sheria 15:10-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mpe kwa ukarimu na ufanye hivyo bila kinyongo moyoni, ndipo kwa sababu ya hili BWANA Mungu wenu atakubariki katika kazi zako zote na kwa kila kitu utakachokiwekea mkono wako. Siku zote watakuwa watu maskini katika nchi. Kwa hiyo ninawaamuru mwe wakarimu kwa ndugu zenu walio maskini na wahitaji katika nchi yenu.