Kumbukumbu la Sheria 11:29-32
Kumbukumbu la Sheria 11:29-32 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu atakapowafikisha kwenye nchi mnayokwenda kuimiliki, mtatangaza baraka kutoka mlima Gerizimu, na laana kutoka mlima Ebali. (Milima hii iko ngambo ya mto Yordani, magharibi ya barabara kuelekea machweo ya jua, katika nchi ya Wakanaani waishio Araba mkabala wa Gilgali). Itawabidi kuvuka mto Yordani mwingie kuimiliki nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapeni. Basi, mtakapoimiliki na kukaa humo, muwe waangalifu kutimiza masharti yote na maagizo ninayowapa leo.
Kumbukumbu la Sheria 11:29-32 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena itakuwa, atakapokuleta BWANA, Mungu wako, na kukutia katika nchi uendeayo kuimiliki, ndipo uiweke baraka juu ya mlima wa Gerizimu, na laana uiweke juu ya mlima wa Ebali. Je! Haiwi ng'ambo ya Yordani? Nyuma ya njia ya machweo ya jua, katika nchi ya Wakanaani waishio katika Araba kuelekea Gilgali, kando ya hiyo mialoni ya More? Kwani ninyi mtavuka Yordani mwingie kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, nanyi muimiliki na kuketi humo. Nanyi angalieni mzifanye amri na hukumu zote niwawekeazo leo mbele yenu.
Kumbukumbu la Sheria 11:29-32 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena itakuwa, atakapokuleta BWANA, Mungu wako, na kukutia katika nchi uendeayo kuimiliki, ndipo uiweke baraka juu ya mlima wa Gerizimu, na laana uiweke juu ya mlima wa Ebali. Je! Haiwi ng’ambo ya Yordani? Nyuma ya njia ya machweo ya jua, katika nchi ya Wakanaani waketio katika Araba kuelekea Gilgali, kando ya hiyo mialoni ya More? Kwani ninyi mtavuka Yordani mwingie kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, nanyi muimiliki na kuketi humo. Nanyi angalieni mzifanye amri na hukumu zote niwawekeazo leo mbele yenu.
Kumbukumbu la Sheria 11:29-32 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wakati BWANA Mungu wenu atakapokuwa amewaleta katika nchi mnayoiingia kuimiliki, mtatangaza baraka kutoka Mlima Gerizimu, na kutangaza laana kutoka Mlima Ebali. Kama mnavyofahamu, milima hii ipo ngʼambo ya Yordani, magharibi ya barabara, kuelekea machweo ya jua, karibu na miti mikubwa ya More, katika nchi ya wale Wakanaani wanaoishi Araba, jirani na Gilgali. Karibu mvuke ngʼambo ya Yordani kuingia na kuimiliki nchi ambayo BWANA Mungu wenu anawapa. Wakati mtakapokuwa mmeichukua na mnaishi humo, hakikisheni kwamba mnatii amri na sheria zote ninazoziweka mbele yenu leo.