Wakolosai 4:2-4
Wakolosai 4:2-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Dumuni katika sala, na mnaposali muwe waangalifu, mkimshukuru Mungu. Vilevile, mtuombee sisi pia ili Mungu atupe fursa ya kuuhubiri ujumbe wake kuhusu siri ya Kristo. Kwa ajili hiyo mimi niko sasa kifungoni. Basi, ombeni ili niweze kusema kama inavyonipasa na kwa namna itakayodhihirisha siri hiyo.
Wakolosai 4:2-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba mkiwa na shukrani; mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa, ili niidhihirishe, kama inipasavyo kunena.
Wakolosai 4:2-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani; mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa, ili niidhihirishe, kama inipasavyo kunena.
Wakolosai 4:2-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru. Pia tuombeeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango wa kunena neno lake, ili tupate kuitangaza siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa. Ombeni ili nipate kuitangaza hiyo siri kwa udhahiri kama inipasavyo.