Amosi 2:4-5
Amosi 2:4-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Watu wa Yuda wametenda dhambi tena na tena, kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu. Wamepuuza sheria zangu, wala hawakufuata amri zangu. Wamepotoshwa na miungu ileile waliyoihudumia wazee wao. Basi, nitaishushia moto nchi ya Yuda, na kuziteketeza kabisa ngome za Yerusalemu.”
Amosi 2:4-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Yuda, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA; wala hawakuzishika amri zake; na maneno yao ya uongo yamewakosesha, ambayo baba zao waliyafuata; lakini nitatuma moto juu ya Yuda, nao utayateketeza majumba ya Yerusalemu. Hukumu kwa Israeli.
Amosi 2:4-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Yuda, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA; wala hawakuzishika amri zake; na maneno yao ya uongo yamewakosesha, ambayo baba zao waliyafuata; lakini nitapeleka moto juu ya Yuda, nao utayateketeza majumba ya Yerusalemu.
Amosi 2:4-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hili ndilo asemalo BWANA: “Kwa dhambi tatu za Yuda, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu wameikataa sheria ya BWANA na hawakuzishika amri zake, kwa sababu wamepotoshwa na miungu ya uongo, miungu ambayo babu zao waliifuata. Nitatuma moto juu ya Yuda ambao utateketeza ngome za Yerusalemu.”