Matendo 27:41-42 - Compare All Versions
Matendo 27:41-42 BHN (Biblia Habari Njema)
Lakini walifika mahali ambapo mikondo miwili ya bahari hukutana, na meli ikakwama. Sehemu ya mbele ilikuwa imezama mchangani bila kutikisika. Sehemu ya nyuma ya meli ilianza kuvunjika vipandevipande kwa mapigo ya nguvu ya mawimbi. Askari walitaka kuwaua wafungwa wote kwa kuogopa kwamba wangeogelea hadi pwani na kutoroka.
Matendo 27:41-42 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Lakini wakafikia mahali palipokutana bahari mbili, wakaiegesha merikebu, omo ikakwama ikakaa isitikiswe, bali tezi ilikuwa imefumuliwa kwa nguvu za mawimbi. Mpango wa askari ulikuwa kuwaua wafungwa, mtu asiogelee na kukimbia.
Matendo 27:41-42 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wakafikia mahali palipokutana bahari mbili, wakaiegesha merikebu, omo ikakwama ikakaa isitikiswe, bali tezi ilikuwa imefumuliwa kwa nguvu za mawimbi. Shauri la askari lilikuwa kuwaua wafungwa, mtu asiogelee na kukimbia.
Matendo 27:41-42 NEN (Neno)
Lakini wakafika mahali bahari mbili zinakutana, wakaipweleza meli ufuoni; omo ikakwama sana, ikawa haiwezi kuondolewa; lakini sehemu ya shetri ikavunjika vipande vipande kutokana na kupigwa kwa mawimbi yenye nguvu. Wale askari wakapanga kuwaua wale wafungwa ili kuzuia hata mmoja wao asiogelee na kutoroka.