Matendo 27:31-32 - Compare All Versions
Matendo 27:31-32 BHN (Biblia Habari Njema)
Lakini Paulo alimwambia yule ofisa wa jeshi na askari wake, “Kama wanamaji hawa hawabaki ndani ya meli, hamtaokoka.” Hapo wale askari walizikata kamba zilizokuwa zimeshikilia ule mtumbwi, wakauacha uchukuliwe na maji.
Shirikisha
Matendo 27 BHNMatendo 27:31-32 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Paulo akawaambia ofisa na askari, Hawa wasipokaa ndani ya merikebu hamtaweza kuokoka. Basi askari wakazikata kamba za mashua, wakaiacha ianguke.
Shirikisha
Matendo 27 SRUVMatendo 27:31-32 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Paulo akawaambia akida na askari, Hawa wasipokaa ndani ya merikebu hamtaweza kuokoka. Basi askari wakazikata kamba za mashua, wakaiacha ianguke.
Shirikisha
Matendo 27 SUVMatendo 27:31-32 NEN (Neno)
Ndipo Paulo akamwambia yule jemadari na askari, “Hawa watu wasipobaki katika meli, hamtaweza kuokoka.” Hivyo basi wale askari wakakata kamba zilizoshikilia ile mashua ya kuokolea watu kwenye meli, wakaiacha ianguke humo baharini.
Shirikisha
Matendo 27 NEN