Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo 27:24-25 - Compare All Versions

Matendo 27:24-25 BHN (Biblia Habari Njema)

akaniambia: ‘Paulo, usiogope! Ni lazima utasimama mbele ya Kaisari; naye Mungu, kwa wema wake, amekufadhili kwa kuwaokoa wote wanaosafiri nawe wasiangamie.’ Hivyo, waheshimiwa, jipeni moyo! Maana ninamwamini Mungu kwamba itakuwa sawa kama nilivyoambiwa.

Shirikisha
Matendo 27 BHN

Matendo 27:24-25 SRUV (Swahili Revised Union Version)

akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.

Shirikisha
Matendo 27 SRUV

Matendo 27:24-25 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. Basi, wanaume, changamkeni; kwa sababu namwamini Mungu, ya kwamba yatakuwa vile vile kama nilivyoambiwa.

Shirikisha
Matendo 27 SUV

Matendo 27:24-25 NEN (Neno)

akaniambia, ‘Paulo usiogope, kwa kuwa ni lazima usimame mbele ya Kaisari, naye Mungu amekupa kwa neema uhai wa wote wanaosafiri pamoja nawe.’ Hivyo jipeni moyo, enyi watu, kwa kuwa ninamwamini Mungu kwamba yatakuwa kama vile alivyoniambia.

Shirikisha
Matendo 27 NEN