Matendo 23:28-29
Matendo 23:28-29 Biblia Habari Njema (BHN)
Nilimpeleka mbele ya Baraza lao kuu nikitaka kujua kisa cha mashtaka yao. Niligundua kwamba mashtaka yenyewe yalihusu ubishi juu ya sehemu kadha wa kadha za sheria yao na hivyo sikuona kwamba amefanya chochote kinachostahili auawe au afungwe gerezani.
Matendo 23:28-29 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nami nikitaka kulijua lile neno walilomshitakia, nikamteremsha nikamweka mbele ya baraza; nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao, wala hakushitakiwa neno lolote la kustahili kuuawa wala kufungwa.
Matendo 23:28-29 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nami nikitaka kulijua lile neno walilomshitakia, nikamtelemsha nikamweka mbele ya baraza; nikaona kwamba ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao, wala hakushitakiwa neno lo lote la kustahili kuuawa wala kufungwa.
Matendo 23:28-29 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nilitaka kujua kwa nini walikuwa wanamshutumu, hivyo nikamleta mbele ya baraza lao. Ndipo nikaona kuwa alikuwa anashutumiwa kwa mambo yanayohusu sheria yao, lakini hakuwa ameshtakiwa kwa jambo lolote linalostahili kifo au kifungo.