Matendo 22:2-3
Matendo 22:2-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Waliposikia akiongea nao kwa Kiebrania wakazidi kukaa kimya zaidi kuliko hapo awali. Naye Paulo akaendelea kusema, “Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso katika Kilikia. Lakini nililelewa papa hapa mjini Yerusalemu chini ya mkufunzi Gamalieli. Nilifundishwa kufuata kwa uthabiti sheria ya wazee wetu. Nilijitolea kwa moyo wote kwa Mungu kama nyinyi wenyewe mlivyo hivi leo.
Matendo 22:2-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Waliposikia kwamba anasema nao kwa lugha ya Kiebrania wakazidi kunyamaza; akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nilizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihada kubwa kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi
Matendo 22:2-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Waliposikia kwamba anasema nao kwa lugha ya Kiebrania wakazidi kunyamaza; akasema, Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi
Matendo 22:2-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Waliposikia akisema kwa lugha ya Kiebrania, wakanyamaza kabisa. Ndipo Paulo akasema, “Mimi ni Myahudi, niliyezaliwa Tarso huko Kilikia, lakini nimelelewa katika mji huu. Miguuni mwa Gamalieli, nilifundishwa kikamilifu katika sheria ya baba zetu, na nikawa mwenye juhudi kwa ajili ya Mungu kama nyote mlivyo leo.