Matendo 21:10-11
Matendo 21:10-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya kukaa huko siku kadhaa, nabii mmoja aitwaye Agabo alifika kutoka Yudea. Alitujia, akachukua mkanda wa Paulo, akajifunga mikono na miguu, akasema, “Roho Mtakatifu asema hivi: ‘Wayahudi kule Yerusalemu watamfunga namna hii mtu mwenye mkanda huu na kumtia mikononi mwa watu wa mataifa.’”
Matendo 21:10-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Yudea. Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.
Matendo 21:10-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Uyahudi. Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.
Matendo 21:10-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Baada ya kukaa kwa siku kadhaa, nabii aliyeitwa Agabo akateremka kutoka Yudea. Alipotufikia, akachukua mshipi wa Paulo, akajifunga, akautumia kufunga mikono na miguu yake mwenyewe, akasema, “Roho Mtakatifu anasema: ‘Hivi ndivyo viongozi wa Wayahudi huko Yerusalemu watakavyomfunga mwenye mshipi huu na kumkabidhi kwa watu wa Mataifa.’ ”