Matendo 20:36-38
Matendo 20:36-38 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya kusema hayo, Paulo alipiga magoti pamoja nao wote, akasali. Wote walikuwa wanalia, na kumwaga kwa kumkumbatia na kumbusu. Jambo lililowahuzunisha zaidi lilikuwa neno alilosema kwamba hawangemwona tena. Basi, wakamsindikiza hadi melini.
Matendo 20:36-38 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Alipokwisha kunena haya akapiga magoti, akaomba pamoja nao wote. Wakalia sana wote, wakamwangukia Paulo shingoni, wakambusubusu, wakihuzunika zaidi kwa sababu ya neno lile alilosema, ya kwamba hawatamwona uso tena. Wakamsindikiza hata merikebuni.
Matendo 20:36-38 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Alipokwisha kunena haya akapiga magoti, akaomba pamoja nao wote. Wakalia sana wote, wakamwangukia Paulo shingoni, wakambusu-busu, wakihuzunika zaidi kwa sababu ya neno lile alilosema, ya kwamba hawatamwona uso tena. Wakamsindikiza hata merikebuni.
Matendo 20:36-38 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Paulo alipomaliza kusema haya akapiga magoti pamoja nao wote akaomba. Wote wakalia, wakamkumbatia Paulo na kumbusu, Kilichowahuzunisha zaidi ni kwa sababu ya yale maneno aliyosema kwamba kamwe hawatauona uso wake tena. Wakaenda naye mpaka kwenye meli.