Matendo 20:10-12
Matendo 20:10-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini Paulo alishuka chini, akainama, akamkumbatia na kusema, “Msiwe na wasiwasi maana kuna uhai bado ndani yake.” Kisha akapanda tena ghorofani, akamega mkate, akala. Aliendelea kuhubiri kwa muda mrefu hadi alfajiri, halafu akaondoka. Wale watu walimchukua yule kijana hadi nyumbani akiwa mzima kabisa, wakapata kitulizo kikubwa.
Matendo 20:10-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Paulo akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema, Msifanye ghasia, maana uzima wake ungalimo ndani yake. Akapanda juu tena, akamega mkate, akala, akazidi kuongea nao hadi alfajiri, ndipo akaenda zake. Wakamleta yule kijana, akiwa mzima, wakafarijika faraja kubwa sana.
Matendo 20:10-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Paulo akashuka, akamwangukia, akamkumbatia, akasema, Msifanye ghasia, maana uzima wake ungalimo ndani yake. Akapanda juu tena, akamega mkate, akala, akazidi kuongea nao hata alfajiri, ndipo akaenda zake. Wakamleta yule kijana, yu mzima, wakafarijika faraja kubwa sana.
Matendo 20:10-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Paulo akashuka chini, akajitupa juu yake na kumkumbatia, akasema, “Msishtuke, bado yuko hai!” Kisha Paulo akapanda tena ghorofani, akamega mkate na kula. Baada ya kuongea hadi mapambazuko, akaondoka. Watu wakamrudisha yule kijana nyumbani akiwa hai nao wakafarijika sana.