Matendo 19:17-18
Matendo 19:17-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Kila mtu huko Efeso, Myahudi na asiye Myahudi, alisikia juu ya tukio hilo. Wote waliingiwa na hofu, wakalitukuza jina la Bwana Yesu. Waumini wengi walijitokeza wakakiri hadharani mambo waliyokuwa wametenda.
Matendo 19:17-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Habari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wagiriki waliokaa Efeso, hofu ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa. Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao.
Matendo 19:17-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Habari hii ikajulikana na Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawaingia wote, na jina la Bwana Yesu likatukuzwa. Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao.
Matendo 19:17-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Habari hii ikajulikana kwa Wayahudi wote na Wayunani waliokaa Efeso, hofu ikawajaa wote, nalo jina la Bwana Yesu likaheshimiwa sana. Wengi wa wale waliokuwa wameamini wakati huu wakaja na kutubu waziwazi kuhusu matendo yao maovu.