Matendo 14:16-18
Matendo 14:16-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Zamani Mungu aliruhusu kila taifa lifanye lilivyopenda. Hata hivyo, Mungu hakuacha kujidhihirisha kwa mambo mema anayowatendea: Huwanyeshea mvua toka angani, huwapa mavuno kwa wakati wake, huwapa chakula na kuijaza mioyo yenu furaha.” Ingawa walisema hivyo haikuwa rahisi kuwazuia wale watu wasiwatambikie.
Matendo 14:16-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
ambaye zamani zilizopita aliwaacha mataifa yote waende katika njia zao wenyewe. Lakini hakujiacha pasipo ushuhuda, kwa kuwa alitenda mema, akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno, akiwashibisha mioyo yenu chakula na furaha. Na kwa maneno hayo wakawazuia watu kwa shida, wasiwatolee dhabihu.
Matendo 14:16-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
ambaye zamani zilizopita aliwaacha mataifa yote waende katika njia zao wenyewe. Lakini hakujiacha pasipo ushuhuda, kwa kuwa alitenda mema, akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno, akiwashibisha mioyo yenu chakula na furaha. Na kwa maneno hayo wakawazuia makutano kwa shida, wasiwatolee dhabihu.
Matendo 14:16-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Zamani aliwaachia mataifa waishi walivyotaka. Lakini hakuacha kuwaonesha watu uwepo wake: Ameonesha wema kwa kuwanyeshea mvua toka mbinguni na kuwapa mazao kwa majira yake, naye amewapa chakula tele na kuijaza mioyo yenu na furaha.” Hata kwa maneno haya yote, ilikuwa vigumu kuzuia umati ule wa watu kuwatolea dhabihu.