2 Timotheo 4:6-8
2 Timotheo 4:6-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa upande wangu mimi, niko karibu kabisa kutolewa tambiko na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimefanya bidii katika mashindano, nimemaliza safari yote na imani nimeitunza. Na sasa imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu, tuzo ambalo Bwana, Hakimu wa haki, atanipa mimi siku ile, na wala si mimi tu, ila na wale wote wanaotazamia kwa upendo kutokea kwake.
2 Timotheo 4:6-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa maana, mimi sasa namiminwa kama tambiko, na wakati wa kuondoka kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji la haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
2 Timotheo 4:6-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.
2 Timotheo 4:6-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa maana mimi sasa ni tayari kumiminwa kama sadaka ya kinywaji, nayo saa yangu ya kuondoka imetimia. Nimevipiga vita vizuri, mashindano nimeyamaliza, imani nimeilinda. Sasa nimewekewa taji la haki ambalo Bwana, Mwamuzi wa haki, atanitunukia siku ile: wala si mimi tu, bali pia wote ambao wamengoja kwa shauku kudhihirishwa kwake.