2 Timotheo 4:5-7
2 Timotheo 4:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Wewe, lakini, uwe macho katika kila hali; vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Habari Njema, timiza kikamilifu utumishi wako. Kwa upande wangu mimi, niko karibu kabisa kutolewa tambiko na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimefanya bidii katika mashindano, nimemaliza safari yote na imani nimeitunza.
2 Timotheo 4:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Bali wewe, uwe mwenye kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza huduma yako kwa ukamilifu. Kwa maana, mimi sasa namiminwa kama tambiko, na wakati wa kuondoka kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda
2 Timotheo 4:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako. Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda
2 Timotheo 4:5-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Bali wewe, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza wajibu wote wa huduma yako. Kwa maana mimi sasa ni tayari kumiminwa kama sadaka ya kinywaji, nayo saa yangu ya kuondoka imetimia. Nimevipiga vita vizuri, mashindano nimeyamaliza, imani nimeilinda.