Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Timotheo 2:5-7 - Compare All Versions

2 Timotheo 2:5-7 BHN (Biblia Habari Njema)

Mwanariadha yeyote hawezi kushinda na kupata zawadi ya ushindi kama asipozitii sheria za michezo. Mkulima ambaye amefanya kazi ngumu anastahili kupata sehemu ya kwanza ya mavuno. Fikiria hayo ninayosema, kwani Bwana atakuwezesha uelewe kila kitu.

2 Timotheo 2:5-7 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali. Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la matunda. Yafahamu sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.

2 Timotheo 2:5-7 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Hata mwanariadha hapewi taji, asiposhindana kwa kufuata sheria. Yampasa mkulima mwenye bidii ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la mavuno. Yatafakari sana hayo nisemayo, kwa maana Bwana atakupa ufahamu katika mambo yote.

2 Timotheo 2:5-7 NEN (Neno)

Vivyo hivyo, mwanariadha hawezi kupewa tuzo ya ushindi asiposhindana kulingana na kanuni za mashindano. Mkulima mwenye bidii ya kazi ndiye anayestahili kuwa wa kwanza kupata fungu la mavuno. Fikiri sana kuhusu haya nisemayo, kwa maana Bwana atakupa ufahamu katika mambo haya yote.