2 Timotheo 2:11-13
2 Timotheo 2:11-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Usemi huu ni wa kweli: “Ikiwa tulikufa pamoja naye, tutaishi pia pamoja naye. Tukiendelea kuvumilia, tutatawala pia pamoja naye. Tukimkana, naye pia atatukana. Tukikosa kuwa waaminifu, yeye hubaki mwaminifu daima, maana yeye hawezi kujikana mwenyewe.”
2 Timotheo 2:11-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana, Kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia; Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi; Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.
2 Timotheo 2:11-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana, Kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia; Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi; Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.
2 Timotheo 2:11-13 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Hili ni neno la kuaminiwa: Kama tumekufa pamoja naye, tutaishi pia pamoja naye. Kama tukistahimili, pia tutatawala pamoja naye. Kama tukimkana, naye atatukana. Tusipoaminika, yeye hudumu akiwa mwaminifu, kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.