2 Wathesalonike 3:16-18
2 Wathesalonike 3:16-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Bwana mwenyewe ambaye ndiye chanzo cha amani, awajalieni amani siku zote kwa kila namna. Bwana awe nanyi nyote. Kwa mkono wangu mwenyewe naandika hivi: Salamu kutoka kwa Paulo! Hivi ndivyo ninavyotia sahihi kila barua; ndivyo ninavyoandika. Tunawatakieni nyote neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.
2 Wathesalonike 3:16-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote. Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika kila barua yangu, ndio mwandiko wangu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote.
2 Wathesalonike 3:16-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sasa, Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote. Bwana awe pamoja nanyi nyote. Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndiyo alama katika kila waraka, ndio mwandiko wangu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote.
2 Wathesalonike 3:16-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Basi, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa kila njia. Bwana awe nanyi nyote. Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote. Hivi ndivyo niandikavyo. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote. Amen.