2 Wathesalonike 1:9-10
2 Wathesalonike 1:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Adhabu yao itakuwa kuangamizwa milele na kutengwa mbali na utukufu wake mkuu, wakati atakapokuja siku ile kupokea utukufu kutoka kwa watu wake na heshima kutoka kwa wote wanaoamini. Nyinyi pia mtakuwa miongoni mwao, kwani mmeuamini ule ujumbe tuliowaletea.
2 Wathesalonike 1:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake; yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu).
2 Wathesalonike 1:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake; yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu).
2 Wathesalonike 1:9-10 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Wataadhibiwa kwa uangamivu wa milele na kutengwa na uso wa Mwenyezi Mungu na utukufu wa uweza wake, siku hiyo atakapokuja kutukuzwa katika watakatifu wake na kustaajabiwa miongoni mwa wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu.