2 Wathesalonike 1:6-7
2 Wathesalonike 1:6-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu atafanya jambo la haki: Atawalipa mateso wale wanaowatesa nyinyi na kuwapeni nafuu nyinyi mnaoteseka, na sisi pia. Atafanya jambo hilo wakati Bwana atakapotokea kutoka mbinguni pamoja na malaika wake wenye nguvu
2 Wathesalonike 1:6-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi; na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake
2 Wathesalonike 1:6-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi; na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake
2 Wathesalonike 1:6-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mungu ni mwenye haki: yeye atawalipa mateso wale wanaowatesa ninyi, na kuwapa ninyi mnaoteseka amani pamoja na sisi, wakati Bwana Yesu atadhihirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu.