2 Samueli 6:14-16
2 Samueli 6:14-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Daudi akiwa amejifunga kizibao cha kuhani kiunoni mwake alicheza kwa nguvu zake zote mbele ya Mwenyezi-Mungu. Hivyo, yeye na Waisraeli wote walilipeleka sanduku la Mwenyezi-Mungu hadi mjini mwa Daudi kwa shangwe na sauti kubwa ya tarumbeta. Sanduku la Mwenyezi-Mungu lilipokuwa linaingia katika mji wa Daudi, Mikali binti Shauli alichungulia dirishani akamwona mfalme Daudi akirukaruka na kucheza mbele ya Mwenyezi-Mungu; basi, akamdharau moyoni mwake.
2 Samueli 6:14-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Daudi akacheza mbele za BWANA kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani. Basi Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalileta sanduku la BWANA kwa shangwe, na kwa sauti ya tarumbeta. Ikawa, sanduku la BWANA lilipoingia mji wa Daudi, Mikali binti Sauli, akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi akirukaruka na kucheza mbele za BWANA; akamdharau moyoni mwake.
2 Samueli 6:14-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Daudi akacheza mbele za BWANA kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani. Basi Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalileta sanduku la BWANA kwa shangwe, na kwa sauti ya tarumbeta. Ikawa, sanduku la BWANA lilipoingia mji wa Daudi Mikali, binti Sauli, akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi akiruka-ruka na kucheza mbele za BWANA; akamdharau moyoni mwake.
2 Samueli 6:14-16 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Daudi, akiwa amevaa kizibau cha kitani, alicheza mbele za BWANA kwa nguvu zake zote, wakati yeye na nyumba yote ya Israeli walipopandisha Sanduku la BWANA kwa shangwe na sauti za tarumbeta. Sanduku la BWANA lilipokuwa linaingia Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani. Naye alipomwona Mfalme Daudi akirukaruka na kucheza mbele za BWANA, akamdharau moyoni mwake.