2 Samueli 4:5-8
2 Samueli 4:5-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Rekabu na Baana wana wa Rimoni Mbeerothi, wakaenda nyumbani kwa Ishboshethi. Walifika huko adhuhuri, Ishboshethi alipokuwa anapumzika nyumbani kwake. Waliingia nyumbani wakijifanya kana kwamba wanataka kuchukua ngano, wakamkuta Ishboshethi amelala kitandani mwake ndani ya chumba chake cha kulala, wakamchoma mkuki tumboni. Baada ya kumwua hivyo hao ndugu wawili walimkata kichwa wakatoroka wakiwa wamekichukua. Walipitia njia ya Araba, wakasafiri usiku kucha. Halafu walichukua kichwa cha Ishboshethi na kumpelekea Daudi huko Hebroni. Nao wakamwambia mfalme Daudi, “Hiki ni kichwa cha Ishboshethi mwana wa Shauli ambaye ni adui yako, aliyekuwa anataka kuyaangamiza maisha yako. Mwenyezi-Mungu leo amekulipizia kisasi dhidi ya Shauli na wazawa wake.”
2 Samueli 4:5-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na wale wana wa Rimoni, Mbeerothi, Rekabu na Baana, wakaenda wakafika nyumbani kwa Ishboshethi, wakati wa joto la mchana, alipokuwa akipumzika adhuhuri. Wakafikia kati ya nyumba, kana kwamba wanataka kuchukua ngano, wakampiga mkuki wa tumbo; kisha Rekabu na Baana nduguye wakakimbia. Basi walipoingia katika ile nyumba, alipokuwa amelala kitandani mwake, katika chumba chake cha kulala, wakampiga, wakamwua, wakamkata kichwa, wakachukua kichwa chake, wakaenda zao kwa njia ya Araba usiku kucha. Wakamletea Daudi kichwa cha Ishboshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, Tazama, hiki ni kichwa cha Ishboshethi, mwana wa Sauli, adui yako, aliyekutafuta roho yako; BWANA amemlipia kisasi bwana wangu mfalme hivi leo, juu ya Sauli, na juu ya wazao wake.
2 Samueli 4:5-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na wale wana wa Rimoni, Mbeerothi, Rekabu na Baana, wakaenda wakafika nyumbani kwa Ishboshethi, wakati wa hari ya mchana, alipokuwa akipumzika adhuhuri. Wakafikia kati ya nyumba, kana kwamba wanataka kuchukua ngano, wakampiga mkuki wa tumbo; kisha Rekabu na Baana nduguye wakakimbia. Basi walipoingia katika ile nyumba, alipokuwa amelala kitandani mwake, katika chumba chake cha kulala, wakampiga, wakamwua, wakamkata kichwa, wakachukua kichwa chake, wakaenda zao kwa njia ya Araba usiku kucha. Wakamletea Daudi kichwa cha Ishboshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, Tazama, hiki ni kichwa cha Ishboshethi, mwana wa Sauli, adui yako, aliyekutafuta roho yako; BWANA amemlipia kisasi bwana wangu mfalme hivi leo, juu ya Sauli, na juu ya wazao wake.
2 Samueli 4:5-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Basi Rekabu na Baana, wana wa Rimoni Mbeerothi wakaenda nyumbani mwa Ish-Boshethi; walifika huko alipokuwa kwenye mapumziko yake ya mchana. Wakaingia kwenye chumba cha ndani kana kwamba wanachukua ngano, wakamchoma Ish-Boshethi mkuki tumboni. Ndipo Rekabu na Baana nduguye wakatoroka. Walikuwa wameingia ndani ya nyumba alipokuwa amelala kitandani chumbani kwake. Baada ya kumchoma mkuki na kumuua, walikata kichwa chake. Walikibeba na kutembea usiku kucha kwa njia ya Araba. Wakamletea Daudi kichwa cha Ish-Boshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, “Hiki hapa kichwa cha Ish-Boshethi mwana wa Sauli, adui yako, aliyejaribu kukuua. Siku hii ya leo BWANA amemlipizia kisasi mfalme bwana wangu dhidi ya Sauli na uzao wake.”