2 Samueli 22:5-7
2 Samueli 22:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
“Maana mawimbi ya kifo yalinizingira, mafuriko ya maangamizi yalinivamia; kamba za kuzimu zilinizinga, mitego ya kifo ilinikabili. “Katika taabu yangu, nilimwita Mwenyezi-Mungu; nilimwita Mungu wangu. Toka hekaluni mwake aliisikia sauti yangu, kilio changu kilimfikia masikioni mwake.
2 Samueli 22:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nilimwita BWANA, Naam, nikamlalamikia Mungu wangu; Naye akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake.
2 Samueli 22:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nalimwita BWANA, Naam, nikamlalamikia Mungu wangu
2 Samueli 22:5-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea. Kamba za Kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili. “Katika shida yangu nalimwita BWANA, nilimlilia Mungu wangu. Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika masikioni mwake.