2 Samueli 22:21-25
2 Samueli 22:21-25 Biblia Habari Njema (BHN)
“Mwenyezi-Mungu alinipa tuzo kadiri ya uadilifu wangu; alinituza kwa vile mikono yangu haina hatia. Maana, nimefuata njia za Mwenyezi-Mungu, wala sikujitenga na Mungu wangu kwa uovu. Nimeshika maagizo yake yote, sikuacha kufuata masharti yake. Mbele yake sikuwa na hatia, nimejikinga nisiwe na hatia. Mwenyezi-Mungu amenituza kadiri ya uadilifu wangu, yeye anajua usafi wangu.
2 Samueli 22:21-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA alinitendea kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu akanilipa. Maana nimezishika njia za BWANA, Wala sikumwasi Mungu wangu. Maana hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu; Na kuhusu amri zake, sikuziacha. Nami nilikuwa mkamilifu kwake, Nikajilinda na uovu wangu. Basi BWANA amenilipa kulingana na haki yangu; Kulingana na usafi wa mikono yangu mbele zake.
2 Samueli 22:21-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA alinitendea sawasawa na haki yangu; Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa. Maana nimezishika njia za BWANA, Wala sikumwasi Mungu wangu. Maana hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu; Na kwa habari za amri zake, sikuziacha. Nami nalikuwa mkamilifu kwake, Nikajilinda na uovu wangu. Basi BWANA amenilipa sawasawa na haki yangu; Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.
2 Samueli 22:21-25 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“BWANA alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa. Kwa maana nimezishika njia za BWANA; sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu. Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake. Nimekuwa sina hatia mbele zake, nami nimejilinda nisitende dhambi. BWANA amenilipa sawasawa na uadilifu wangu, sawasawa na usafi wangu machoni pake.