2 Wafalme 6:1-7
2 Wafalme 6:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Siku moja, wanafunzi wa manabii walimlalamikia Elisha wakisema, “Mahali hapa tunapokaa ni padogo sana kwetu! Turuhusu twende Yordani tukate miti ili tujijengee mahali patakapotutosha.” Elisha akawajibu, “Nendeni.” Mmoja wao akamwomba akisema, “Tafadhali uwe radhi uende na watumishi wako.” Naye akajibu, “Nitakwenda.” Hivyo akaenda pamoja nao, na walipofika mtoni Yordani wakaanza kukata miti. Mmoja wao alipokuwa anakata miti, shoka lake likachomoka na kuanguka majini; akalia, akisema, “Sasa bwana wangu nitafanya nini? Shoka hili tulikuwa tumeliazima!” Elisha akauliza, “Liliangukia wapi?” Mtu huyo akamwonesha. Elisha akakata kijiti na kukitupa majini na papo hapo shoka likaelea juu ya maji. Elisha akamwamuru alichukue naye akanyosha mkono, akalichukua.
2 Wafalme 6:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha, wana wa manabii wakamwambia Elisha, Angalia basi, mahali tukaapo mbele yako ni padogo kwetu. Basi twende mpaka Yordani, twakuomba, tutwae huko kila mtu mti mmoja, ili tujifanyie huko mahali pa kukaa. Akajibu, Haya! Nendeni. Mmoja wao akasema, Uwe radhi, basi nakusihi, uende pamoja na watumishi wako. Akajibu, Nitakwenda. Basi, akaenda pamoja nao. Nao walipofika Yordani, wakakata miti. Lakini mmojawapo alipokuwa katika kukata boriti, chuma cha shoka kikaanguka majini; akalia, akasema, Ole wangu! Bwana wangu, kwani kiliazimiwa kile. Mtu wa Mungu akasema, Kilianguka wapi? Akamwonesha mahali. Akakata kijiti, akakitupa pale pale, chuma kikaelea. Akasema, Kiokote. Basi akanyosha mkono, akakitwaa.
2 Wafalme 6:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha, wana wa manabii wakamwambia Elisha, Angalia basi, mahali tukaapo mbele yako ni padogo kwetu. Basi twende mpaka Yordani, twakuomba, tutwae huko kila mtu mti mmoja, ili tujifanyie huko mahali pa kukaa. Akajibu, Haya! Nendeni. Mmoja wao akasema, Uwe radhi, basi nakusihi, uende pamoja na watumishi wako. Akajibu, Nitakwenda. Basi, akaenda pamoja nao. Nao walipofika Yordani, wakakata miti. Lakini mmojawapo alipokuwa katika kukata boriti, chuma cha shoka kikaanguka majini; akalia, akasema, Ole wangu! Bwana wangu, kwani kiliazimiwa kile. Mtu wa Mungu akasema, Kilianguka wapi? Akamwonyesha mahali. Akakata kijiti, akakitupa pale pale, chuma kikaelea. Akasema, Kiokote. Basi akanyosha mkono, akakitwaa.
2 Wafalme 6:1-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wana wa manabii wakamwambia Elisha, “Tazama, mahali hapa tunapokutana nawe ni padogo sana kwetu. Twendeni Yordani, ambapo kila mmoja wetu anaweza kupata nguzo moja, nasi tujenge huko mahali petu pa kuishi.” Naye akawaambia, “Nendeni.” Kisha mmoja wao akasema, “Je, tafadhali, huwezi kufuatana na watumishi wako?” Elisha akajibu, “Nitakuja.” Naye akaenda pamoja nao. Basi wakaenda Yordani, nao wakaanza kukata miti. Mmoja wao alipokuwa anakata mti, shoka lilitumbukia kwenye maji. Akalia, “Ee bwana wangu, shoka lilikuwa la kuazima!” Mtu wa Mungu akauliza, “Je, liliangukia wapi?” Alipomwonesha mahali penyewe, Elisha akakata kijiti na kukitupa mahali pale, nalo shoka likaelea. Akasema, “Lichukue.” Kisha yule mtu akanyoosha mkono wake, akalichukua.