2 Wafalme 5:3-5
2 Wafalme 5:3-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Siku moja akamwambia bibi yake, mke wa Naamani, “Laiti bwana wangu angekwenda na kumwona yule nabii aliyeko Samaria! Angemponya ugonjwa wake.” Naamani alipopata habari hizi, akaenda kwa mfalme na kumweleza habari za mtoto huyu. Mfalme wa Aramu akamwambia, “Chukua barua hii umpelekee mfalme wa Israeli.” Hivyo Naamani akaondoka, huku amechukua vipande 30,000 vya fedha, vipande 6,000 vya dhahabu na mavazi kumi ya sikukuu.
2 Wafalme 5:3-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake. Mtu mmoja akaingia, akamwambia bwana wake, akasema, Yule kijana mwanamke aliyetoka nchi ya Israeli asema hivi na hivi. Mfalme wa Shamu akasema, Haya! Basi, mimi nitampelekea mfalme wa Israeli waraka. Basi akaenda zake, akachukua mikononi mwake talanta kumi za fedha, na vipande vya dhahabu elfu sita, na mavazi kumi.
2 Wafalme 5:3-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake. Mtu mmoja akaingia, akamwambia bwana wake, akasema, Yule kijana mwanamke aliyetoka nchi ya Israeli asema hivi na hivi. Mfalme wa Shamu akasema, Haya! Basi, mimi nitampelekea mfalme wa Israeli waraka. Basi akaenda zake, akachukua mikononi mwake talanta kumi za fedha, na vipande vya dhahabu elfu sita, na mavazi kumi.
2 Wafalme 5:3-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Akamwambia bibi yake, “Kama bwana wangu angemwona nabii aliye huko Samaria! Angemponya ukoma wake.” Naamani akaenda kwa bwana wake na kumwambia alichosema yule msichana kutoka Israeli. Mfalme wa Aramu akamjibu, “Hakika, nenda. Nitatuma barua kwa mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo Naamani akaondoka, akiwa amechukua talanta kumi za fedha, shekeli elfu sita za dhahabu, na mavazi kumi.