2 Wafalme 19:5-7
2 Wafalme 19:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, hao watumishi wa mfalme Hezekia walipokwisha fika kwa Isaya, aliwaambia “Mwambieni bwana wenu kwamba Mwenyezi-Mungu asema hivi, ‘Usiogope kwa sababu ya maneno uliyoyasikia, ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wameyasema kunikebehi. Tazama nitamfanya mfalme asikie uvumi, halafu atarudi katika nchi yake na huko nitamfanya auawe kwa upanga.’”
2 Wafalme 19:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi watumishi wa mfalme Hezekia wakamwendea Isaya. Isaya akawaambia, Mwambieni bwana wenu maneno haya; BWANA asema hivi, Usiyaogope maneno hayo uliyoyasikia, ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana. Tazama, nitatia roho ya hofu ndani yake, naye atasikia uvumi, na kuirudia nchi yake mwenyewe; nami nitamwangusha kwa upanga katika nchi yake mwenyewe.
2 Wafalme 19:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi watumishi wa mfalme Hezekia wakamwendea Isaya. Isaya akawaambia, Mwambieni bwana wenu maneno haya; BWANA asema hivi, Usiyaogope maneno hayo uliyoyasikia, ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana. Tazama, nitatia roho ya hofu ndani yake, naye atasikia kivumi, na kuirudia nchi yake mwenyewe; nami nitamwangusha kwa upanga katika nchi yake mwenyewe.
2 Wafalme 19:5-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Maafisa wa Mfalme Hezekia walipofika kwa Isaya, Isaya akawaambia, “Mwambieni bwana wenu, ‘Hili ndilo asemalo BWANA: Usiogope kwa hayo uliyoyasikia, yale maneno ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana nayo. Sikiliza! Nitatia roho fulani ndani yake, naye atakaposikia ujumbe fulani, atarudi nchi yake mwenyewe; nami huko nitafanya auawe kwa upanga.’ ”