2 Wafalme 10:15-16
2 Wafalme 10:15-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Yehu akatoka tena na alipofika njiani akakutana na Yehonadabu mwana wa Rekabu; Yehu akamsalimu, kisha akamwambia “Wewe una mawazo sawa na yangu? Je, utajiunga nami na kunisaidia?” Yehonadabu akamjibu, “Naam, nitajiunga nawe:” Yehu akasema, “Basi, nipe mkono wako.” Wakashikana mikono na Yehu akampandisha garini mwake. Akamwambia, “Fuatana nami ili ujionee jinsi nilivyo mwaminifu kwa Mwenyezi-Mungu.” Basi, wakasafiri pamoja garini mwake.
2 Wafalme 10:15-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Alipotoka huko akamkuta Yehonadabu mwana wa Rekabu akija kumlaki; akamsalimu akamwambia, Je! Moyo wako umenyoka, kama moyo wangu ulivyo pamoja na moyo wako? Akajibu Yehonadabu, Ndio. Yehu akamwambia, Kama ndio, nipe mkono wako. Akampa mkono, akamkalisha pamoja naye garini. Akasema, Fuatana nami, ukaone wivu wangu kwa BWANA. Wakampandisha garini mwake.
2 Wafalme 10:15-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Alipotoka huko akamkuta Yehonadabu mwana wa Rekabu akija kumlaki; akamsalimu akamwambia, Je! Moyo wako umenyoka, kama moyo wangu ulivyo pamoja na moyo wako? Akajibu Yehonadabu, Ndio. Yehu akamwambia, Kama ndio, nipe mkono wako. Akampa mkono, akamkalisha pamoja naye garini. Akasema, Fuatana nami, ukaone wivu wangu kwa BWANA. Wakampandisha garini mwake.
2 Wafalme 10:15-16 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Baada ya kuondoka hapo, alimkuta Yehonadabu mwana wa Rekabu, aliyekuwa akienda kumlaki. Yehu akamsalimu na kusema, “Je, moyo wako ni mnyofu kwangu kama moyo wangu ulivyo kwako?” Yehonadabu akajibu, “Ndiyo.” Yehu akasema, “Kama ndivyo, nipe mkono wako.” Yeye akampa mkono, naye Yehu akampandisha kwenye gari lake la vita. Yehu akasema, “Twende pamoja ukaone wivu wangu kwa ajili ya BWANA.” Hivyo wakasafiri pamoja kwenye gari lake la vita.