2 Yohane 1:1-3
2 Yohane 1:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mimi mzee nakuandikia wewe Bimkubwa mteule pamoja na watoto wako ninaowapenda kweli. Wala si mimi tu ninayewapenda, bali pia wote wanaoujua ule ukweli wanawapenda nyinyi, kwa sababu ukweli unakaa nasi milele. Neema na huruma na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo, Mwana wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika ukweli na upendo.
2 Yohane 1:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuayo ile kweli; kwa ajili ya hiyo kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hata milele. Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwana wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.
2 Yohane 1:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mzee, kwa mama mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na wote waijuao ile kweli; kwa ajili ya hiyo kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hata milele. Neema, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo Mwana wa Baba, zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.
2 Yohane 1:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mzee. Kwa mama mteule na watoto wake, ninaowapenda katika kweli; wala si mimi tu, bali na wale wote wanaoijua kweli; kwa sababu ya ile kweli inayokaa ndani yetu, na ambayo itaendelea kukaa nasi milele. Neema, rehema na amani zinazotoka kwa Mungu Baba na kwa Yesu Kristo, Mwanawe Baba, zitakuwa pamoja nasi katika kweli na upendo.